|
|
Zaburi, Chapter 128
1. Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake.
2. Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.
3. Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.
4. Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.
5. Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
6. Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|