Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 136

Bible Study - Zaburi 136 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
2. Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
3. Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
4. Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
5. Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
6. Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
7. Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
8. Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
9. Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
10. Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
11. Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
12. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
13. Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
14. Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
15. Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
16. Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
17. Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
18. Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
19. Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
20. Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
21. Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
22. Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
23. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
24. Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
25. Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
  
26. Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES