|
|
Zaburi, Chapter 137
1. Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.
2. Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu.
3. Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.
4. Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni?
5. Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe, Mkono wangu wa kuume na usahau.
6. Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.
7. Ee Bwana, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ya Yerusalemu. Waliosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini!
8. Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.
9. Heri yeye atakayewakamata wadogo wako, Na kuwaseta wao juu ya mwamba.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|