|
|
Zaburi, Chapter 148
1. Haleluya. Msifuni Bwana kutoka mbinguni; Msifuni katika mahali palipo juu.
2. Msifuni, enyi malaika wake wote; Msifuni, majeshi yake yote.
3. Msifuni, jua na mwezi; Msifuni, nyota zote zenye mwanga.
4. Msifuni, enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu.
5. Na vilisifu jina la Bwana, Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.
6. Amevithibitisha hata milele na milele, Ametoa amri wala haitapita.
7. Msifuni Bwana kutoka nchi, Enyi nyangumi na vilindi vyote.
8. Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke, Upepo wa dhoruba ulitendao neno lake.
9. Milima na vilima vyote, Miti yenye matunda na mierezi yote.
10. Hayawani, na wanyama wafugwao, Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa.
11. Wafalme wa dunia, na watu wote, Wakuu, na makadhi wote wa dunia.
12. Vijana waume, na wanawali, Wazee, na watoto;
13. Na walisifu jina la Bwana, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.
14. Naye amewainulia watu wake pembe, Sifa za watauwa wake wote; Wana wa Israeli, watu walio karibu naye. Haleluya.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|