Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 149

Bible Study - Zaburi 149 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.
  
2. Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.
  
3. Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie.
  
4. Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
  
5. Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
  
6. Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.
  
7. Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, Na adhabu juu ya kabila za watu.
  
8. Wawafunge wafalme wao kwa minyororo, Na wakuu wao kwa pingu za chuma.
  
9. Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote. Haleluya.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES