|
|
Zaburi, Chapter 20
1. Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.
2. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni.
3. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako.
4. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote.
5. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote.
6. Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake;Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu.
7. Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.
8. Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.
9. Bwana, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|