Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 21

Bible Study - Zaburi 21 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Ee Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.
  
2. Umempa haja ya moyo wake, Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake.
  
3. Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
  
4. Alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele.
  
5. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako, Heshima na adhama waweka juu yake.
  
6. Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako.
  
7. Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa.
  
8. Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia.
  
9. Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala.
  
10. Matunda yao utayaharibu na kuyaondoa katika nchi, Na wazao wao katika wanadamu.
  
11. Madhali walinuia kukutenda mabaya, Waliwaza hila wasipate kuitimiza.
  
12. Kwa maana utawafanya kukupa kisogo, Kwa upote wa uta wako ukiwaelekezea mishale.
  
13. Ee Bwana, utukuzwe kwa nguvu zako, Nasi tutaimba na kuuhimidi uweza wako.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES