|
|
Zaburi, Chapter 3
1. Bwana, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia,
2. Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu.
3. Na Wewe, Bwana, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.
4. Kwa sauti yangu namwita Bwana Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.
5. Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa Bwana ananitegemeza.
6. Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote.
7. Bwana, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki.
8. Wokovu una Bwana; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|