|
|
Zaburi, Chapter 4
1. Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; Umenifanyizia nafasi wakati wa shida; Unifadhili na kuisikia sala yangu.
2. Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo?
3. Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa; Bwana atasikia nimwitapo.
4. Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
5. Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana.
6. Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema? Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
7. Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.
8. Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|