Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 46

Bible Study - Zaburi 46 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
  
2. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
  
3. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
  
4. Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.
  
5. Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
  
6. Mataifa yalighadhibika, falme zikataharuki; Alitoa sauti yake, nchi ikayeyuka.
  
7. Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
  
8. Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
  
9. Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.
  
10. Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
  
11. Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES