|
|
Zaburi, Chapter 47
1. Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.
2. Kwa kuwa Bwana Aliye juu, mwenye kuogofya, Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.
3. Atawatiisha watu wa nchi chini yetu, Na mataifa chini ya miguu yetu.
4. Atatuchagulia urithi wetu, Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda.
5. Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti ya baragumu.
6. Mwimbieni Mungu, naam, imbeni; Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni.
7. Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili.
8. Mungu awamiliki mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.
9. Wakuu wa watu wamekusanyika, Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu. Maana ngao za dunia zina Mungu, Ametukuka sana.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|