Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 49

Bible Study - Zaburi 49 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Sikieni haya, enyi mataifa yote; Sikilizeni, ninyi nyote mnaokaa duniani.
  
2. Watu wakuu na watu wadogo wote pia, Tajiri na maskini wote pamoja.
  
3. Kinywa changu kitanena hekima, Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara.
  
4. Nitatega sikio langu nisikie mithali, Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi
  
5. Kwa nini niogope siku za uovu, Ubaya ukinizunguka miguuni pangu?
  
6. Wa hao wanaozitumainia mali zao, Na kujisifia wingi wa utajiri wao;
  
7. Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake, Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake,
  
8. (Maana fidia ya nafsi zao ina gharama, Wala hana budi kuiacha hata milele;)
  
9. ili aishi sikuzote asilione kaburi.
  
10. Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa; Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja, Na kuwaachia wengine mali zao.
  
11. Makaburi ni nyumba zao hata milele, Maskani zao vizazi hata vizazi. Hao waliotaja mashamba yao Kwa majina yao wenyewe.
  
12. Lakini mwanadamu hadumu katika heshima, Bali amefanana na wanyama wapoteao.
  
13. Hiyo ndiyo njia yao, ujinga wao, Nao walioko baada yao huyaridhia maneno yao.
  
14. Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na mauti itawachunga; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Umbo lao litachakaa, kao lao ni kuzimu.
  
15. Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha.
  
16. Usiogope mtu atakapopata utajiri, Na fahari ya nyumba yake itakapozidi.
  
17. Maana atakapokufa hatachukua cho chote; Utukufu wake hautashuka ukimfuata.
  
18. Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai, Na watu watakusifu ukijitendea mema,
  
19. Atakwenda kwenye kizazi cha baba zake Hawataona nuru hata milele.
  
20. Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili, Amefanana na wanyama wapoteao.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES