|
|
Zaburi, Chapter 48
1. Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.
2. Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu.
3. Mungu katika majumba yake Amejijulisha kuwa ngome.
4. Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walipita wote pamoja.
5. Waliona, mara wakashangaa; Wakafadhaika na kukimbia.
6. Papo hapo tetemeko liliwashika, Utungu kama wa mwanamke azaaye.
7. Kwa upepo wa mashariki Wavunja jahazi za Tarshishi.
8. Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa Bwana wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu ataufanya imara hata milele.
9. Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, Katikati ya hekalu lako.
10. Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu, Ndivyo na sifa yako hata miisho ya dunia. Mkono wako wa kuume umejaa haki;
11. Na ufurahi mlima Sayuni. Binti za Yuda na washangilie Kwa sababu ya hukumu zako.
12. Tembeeni katika Sayuni, Uzungukeni mji, Ihesabuni minara yake,
13. Tieni moyoni boma zake, Yafikirini majumba yake, Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja.
14. Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|