|
|
Zaburi, Chapter 6
1. Bwana, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.
2. Bwana, unifadhili, maana ninanyauka; Bwana, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.
3. Na nafsi yangu imefadhaika sana; Na Wewe, Bwana, hata lini?
4. Bwana urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
5. Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
6. Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza kitanda changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu.
7. Jicho langu limeharibika kwa masumbufu, Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.
8. Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa Bwana ameisikia sauti ya kilio changu.
9. Bwana ameisikia dua yangu; Bwana atayatakabali maombi yangu.
10. Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, Watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|