Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 7

Bible Study - Zaburi 7 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Bwana, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe, Uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye.
  
2. Asije akaipapura nafsi yangu kama simba, Akiivunja-vunja pasipokuwa na wa kuponya.
  
3. Bwana, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya, Ikiwa mna uovu mikononi mwangu,
  
4. Ikiwa nimemlipa mabaya Yeye aliyekaa kwangu salama; (Hasha! Nimemponya yeye Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;)
  
5. Basi adui na anifuatie, Na kuikamata nafsi yangu; Naam, aukanyage uzima wangu, Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.
  
6. Bwana uondoke kwa hasira yako; Ujiinue juu ya jeuri ya watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.
  
7. Kusanyiko la mataifa na likuzunguke, Na juu yake uketi utawale.
  
8. Bwana atawaamua mataifa, Bwana, unihukumu mimi, Kwa kadiri ya haki yangu, Sawasawa na unyofu nilio nao.
  
9. Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na viuno Ndiye Mungu aliye mwenye haki.
  
10. Ngao yangu ina Mungu, Awaokoaye wanyofu wa moyo.
  
11. Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu aghadhibikaye kila siku.
  
12. Mtu asiporejea ataunoa upanga wake; Ameupinda uta wake na kuuweka tayari;
  
13. Naye amemtengenezea silaha za kufisha, Akifanya mishale yake kuwa ya moto.
  
14. Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.
  
15. Amechimba shimo, amelichimba chini sana, Akatumbukia katika handaki aliyoifanya!
  
16. Madhara yake yatamrejea kichwani pake, Na dhuluma yake itamshukia utosini.
  
17. Nitamshukuru Bwana kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la Bwana aliye juu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES