Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 66

Bible Study - Zaburi 66 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,
  
2. Imbeni utukufu wa jina lake, Tukuzeni sifa zake.
  
3. Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.
  
4. Nchi yote itakusujudia na kukuimbia, Naam, italiimbia jina lako.
  
5. Njoni yatazameni matendo ya Mungu; Hutisha kwa mambo awatendayo wanadamu;
  
6. Aligeuza bahari ikawa nchi kavu; Katika mto walivuka kwa miguu; Huko ndiko mlikomfurahia.
  
7. Atawala kwa uweza wake milele; Macho yake yanaangalia mataifa; Waasio wasijitukuze nafsi zao.
  
8. Enyi mataifa, mtukuzeni Mungu wetu, Itangazeni sauti ya sifa zake;
  
9. Aliyeiweka nafsi yetu katika uhai, Wala hakuuacha mguu wetu usogezwe.
  
10. Kwa maana umetupima, Ee Mungu, Umetujaribu inavyojaribiwa fedha.
  
11. Ulituingiza ndani ya wavu, Na kuweka viunoni mwetu mzigo uliotulemea.
  
12. Uliwapandisha watu Juu ya vichwa vyetu. Tulipita motoni na majini; Ukatutoa na kutuleta kunako wingi.
  
13. Nitaingia nyumbani mwako na kafara; Nitaondoa kwako nadhiri zangu;
  
14. Ambazo midomo yangu ilizinena; Kinywa changu kikazisema nilipokuwa taabuni.
  
15. Kafara za vinono nitakutolea, Pamoja na fukizo la kondoo waume, Nitatoa ng'ombe pamoja na mbuzi.
  
16. Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu, Nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.
  
17. Nalimwita kwa kinywa changu, Na sifa kuu zilikuwa chini ya ulimi wangu.
  
18. Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia.
  
19. Hakika Mungu amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu.
  
20. Na ahimidiwe Mungu asiyeyakataa maombi yangu, Wala kuniondolea fadhili zake.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES