|
|
Zaburi, Chapter 67
1. Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake.
2. Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote.
3. Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.
4. Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
5. Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.
6. Nchi imetoa mazao yake MUNGU, Mungu wetu, ametubariki.
7. Mungu atatubariki sisi; Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|