Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 81

Bible Study - Zaburi 81 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo.
  
2. Pazeni zaburi, pigeni matari, Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda.
  
3. Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu.
  
4. Kwa maana ni sheria kwa Israeli, Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo.
  
5. Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu, Alipoondoka juu ya nchi ya Misri; Maneno yake nisiyemjua naliyasikia.
  
6. Nimelitenga bega lake na mzigo, Mikono yake ikaachana na kikapu.
  
7. Katika shida uliniita nikakuokoa; Nalikuitikia katika sitara ya radi; Nalikujaribu penye maji ya Meriba.
  
8. Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya, Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza;
  
9. Usiwe na mungu mgeni ndani yako; Wala usimsujudie mungu mwingine.
  
10. Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.
  
11. Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu, Wala Israeli hawakunitaka.
  
12. Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao, Waenende katika mashauri yao.
  
13. Laiti watu wangu wangenisikiliza, Na Israeli angeenenda katika njia zangu;
  
14. Ningewadhili adui zao kwa upesi, Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu;
  
15. Wamchukiao Bwana wangenyenyekea mbele zake, Bali wakati wao ungedumu milele.
  
16. Naam, ningewalisha kwa unono wa ngano, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES