|
|
Zaburi, Chapter 82
1. Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu.
2. Hata lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya?
3. Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara;
4. Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
5. Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika.
6. Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.
7. Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
8. Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana Wewe utawarithi mataifa yote.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|