Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 9

Bible Study - Zaburi 9 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu;
  
2. Nitafurahi na kukushangilia Wewe; Nitaliimbia jina lako, Wewe Uliye juu.
  
3. Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma; Hujikwaa na kuangamia mbele zako.
  
4. Kwa maana umenifanyia hukumu na haki Umeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki.
  
5. Umewakemea mataifa; Na kumwangamiza mdhalimu; Umelifuta jina lao milele na milele;
  
6. Adui wamekoma na kuachwa ukiwa milele. Nayo miji yao uliing'oa; Hata kumbukumbu lao limepotea.
  
7. Bali Bwana atakaa milele, Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu.
  
8. Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki; Atawaamua watu kwa adili.
  
9. Bwana atakuwa ngome kwake aliyeonewa, Naam, ngome kwa nyakati za shida.
  
10. Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, Bwana hukuwaacha wakutafutao.
  
11. Mwimbieni Bwana akaaye Sayuni, Yatangazeni kati ya watu matendo yake.
  
12. Maana mlipiza kisasi cha damu awakumbuka, Hakukisahau kilio cha wanyonge.
  
13. Wewe, Bwana, unifadhili, Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia; Wewe uniinuaye katika malango ya mauti,
  
14. Ili nizisimulie sifa zako zote; Katika malango ya binti Sayuni Nitaufurahia wokovu wako.
  
15. Mataifa wamezama katika shimo walilolifanya; Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao.
  
16. Bwana amejidhihirisha na kutekeleza hukumu; Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake.
  
17. Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
  
18. Kwa maana mhitaji hatasahauliwa daima; Matumaini ya wanyonge hayatapotea milele.
  
19. Bwana, usimame, mwanadamu asipate nguvu, Mataifa wahukumiwe mbele zako.
  
20. Bwana, uwawekee kitisho, Mataifa na wajijue kuwa ni binadamu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES