|
|
Zaburi, Chapter 8
1. Wewe, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;
2. Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi.
3. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;
4. Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?
5. Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;
6. Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
7. Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni;
8. Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.
9. Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|