Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 91

Bible Study - Zaburi 91 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
  
2. Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
  
3. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
  
4. Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.
  
5. Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,
  
6. Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,
  
7. Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.
  
8. Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.
  
9. Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.
  
10. Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
  
11. Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.
  
12. Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
  
13. Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
  
14. Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
  
15. Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;
  
16. Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES