Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 92

Bible Study - Zaburi 92 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu.
  
2. Kuzitangaza rehema zako asubuhi, Na uaminifu wako wakati wa usiku.
  
3. Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi.
  
4. Kwa kuwa umenifurahisha, Bwana, Kwa kazi yako; nitashangilia Kwa ajili ya matendo ya mikono yako.
  
5. Ee Bwana, jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa.
  
6. Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu.
  
7. Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele;
  
8. Bali Wewe, Bwana, U Mtukufu hata milele.
  
9. Maana hao adui zako, Ee Bwana, Hao adui zako watapotea, Na watendao maovu watatawanyika wote pia.
  
10. Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa mafuta mabichi.
  
11. Na jicho langu limewatazama walioniotea, Sikio langu limesikia habari za waovu walionishambulia.
  
12. Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni.
  
13. Waliopandwa katika nyumba ya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu.
  
14. Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi.
  
15. Watangaze ya kuwa Bwana ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES